-->

Katibu wa Bodi ya Filamu Bi. Fissoo Amtembelea Wankota Nyumbani Kwake

KATIBU wa bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo amemtembelea muandishi wa muswada mwenye kipaji cha ajabu Wankota Kapunda nyumbani kwao Mbezi kwa ajili ya kumtakia heri ya mwaka mpya na kubadilishana naye mawazo kufuatia maandalizi ya utayarishaji wa filamu na tamthilia inayoitwa Uaridi.

Katibu Bi. Joyce Fissoo akiwa katika picha ya furaha na Wankota.

“Mwaka mpya umeanza ni vema kuwaona wadau wetu na pia nimekuja kwa ajili ya Waziri wetu Mh. Nape kukusikiliza unaendelea na project yako ambayo ulipanga kuifanya katika maandalizi ya mwaka jana,”

“Pia nimekuja kwa ajili ya kukutakia heri ya mwaka mpya kama mwanafamilia mwezangu,”

Akiongea na katibu wa Bodi mwandishi huyo mwenye kipaji cha kipekee Wankota alisema kuwa awali alikuwa na filamu ambayo tayari amemaliza kuandika kutokana na ukubwa wa bajeti ameamua kuiweka pembeni kwanza lakini afanye tamthilia ambayo atairusha katika televisheni ya Taifa TBC 1.

“Nashukru sana kwa kuwa pamoja name lakini kuna changamoto ambazo zinanikabiri kwa sasa ambazo nahitaji usaidizi ningeomba kupatiwa Bima ya matibabu, Nyumba ya kuishi hapa tumepanga na mwenyewe anapauza na nahitaji iliyotulia kama hii,”

“Pia nilikuwa nahitaji bajeti ya filamu yangu ambayo ndio ilikuwa ya kwanza kuandika ambayo bajeti yake ilikuwa kama milioni 80 pamoja na gharama za utengenezaji na kusambaza lakini ngoja nianze na tamthilia ambayo nimepata ufadhili TBC 1.

Bi.Fissoo alissema kuwa amepokea changamoto za Wankota na atawakilisha kwa Mh. Waziri kwa zile zenye kuhitaji usaidizi zaidi lakini kuna zile changamoto kama za utayarishaji na maeneo mengi atashughulikia na kupata majibu haraka zaidi katika harakati za kuunga mkono harakati za mwanadada huyo.

Bi. Fissoo akiwa na familia ya Wankota kutoka kushoto ni Baba, Mama na Wankota

“Nitashauriana na Waziri kwa ajili ya mahitaji yako lakini maeneo mengine kama ofisi tutayatua kama suala la bima na pia utatupatia script yako kwa ajili ya kuipitia na kuona jinsi ya kuwaona wadau ambao wanaweza kusaidia kuifanikisha,”

Wankota pamoja na familia yake wamemshukru sana Katibu wa Bodi ya filamu kwa juhudi zake za kuwasapoti kwa kila hatua ambayo kijana wao anaifanya naye katibu aliahidi kumsaidia Wankota katika kuweza kufanikisha ndoto zake katika tasnia ya filamu.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364