-->

Jennifer Mgendi Kuja na albamu Mpya Pamoja na Filamu

Msanii mkongwe wa nyimbo za Injili nchini, Jennifer Mgendi baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu anajipanga kuachia albamu yake mpya iitwayo,’Nyuma ya Mlima’.

Muimbaji huyo ambaye amewahi kutamba na wimbo Mchimba Mashimo, Nalia na nyingine nyingi, amesema kuwa ameamua kuachia albamu hiyo kama zawadi ya kuwatia moyo mashabiki wake wanaopita katika magumu mbalimbali.

“Nina kila sababu ya kufikisha ujumbe ambao Mungu ameweka moyoni mwangu kwa walimwengu juu ya uweza wa Mungu na kwamba atatuvusha katika magumu yote,”

Aliongeza, “Albumu hii ni mwanzo wa ujio wa filamu yangu mpya ya Baba Jackie ambayo imewasilishwa na wimbo wa Tamaa Mbele,”.

Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albumu hiyo ni pamoja na Tamaa Mbele (Baba Jackie), Penda Unapopendwa, Yesu ni Wathamani, Mitihani ya Maisha na Ninamshukuru Adui.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364