-->

Jike Shupa Akataliwa Ukweni

WAKATI akiwa na matumaini kuwa huenda naye akampata wake wa kutengeneza familia yake, muuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amekataliwa na wazazi wa mwanaume aliyetaka kumuoa.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Jike Shupa alisema ataendelea kuishi na mwanaume huyo bila ndoa hata katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu kwa kuwa alivyotegemea imekuwa tofauti.

“Wazazi wa mpenzi wangu walimkataza mtoto wao asifunge ndoa na mimi na wazazi wangu nao walitaka mahari, hivyo ikashindikana, ikabidi tuendelee kuishi tu hivyohivyo kwa hiyo siwezi kufunga wakati kila siku natenda dhambi,” alisema msichana huyo mwingi wa vituko.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364