-->

Rais Magufuli Afunguka Anavyomkumbuka Ndesamburo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa na taarifa za kifo cha Mbunge mstaafu wa Jimbo la Moshi mjini Mzee Philemon Ndesamburo kilichotokea asubuhi ya leo.

Mzee Philemon Ndesamburo

Katika salamu za rambirambi alizozitoa Rais Magufuli kwenda kwa wafiwa pamoja na viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyoko Moshi Mkoani Kilimanjaro. Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu” alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amesema alifanya kazi na marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana huku akimkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslahi kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameitaka familia ya marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huo kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu walichonacho.

Kwa upande mwingine Rais Mgufuli amemuombea dua marehemu apumzishwe mahali pepa peponi.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364