Jina la Mtoto wa Hamisa Mobetto Lazua Utata, Diamond Azidi Kuhusishwa
Mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobetto Jumatatu hii ametimiza siku saba toka azaliwe Agosti 8 mwaka huu ambapo amepewa jina la Abdul Naseeb. Jina ambalo limeanza kumaliza maswali mengi ya mashabiki ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo.
Awali mrembo huyo alifungua akaunti ya Instagram kwa jina ‘Tanzania Baby’ lakini Jumanne hii alibadilisha jina na kuandika ‘Abdul Naseeb’ ambapo kwa sasa akaunti hiyo tayari ina wafuasi zaidi 50,000.
Mobetto kupitia Instagram alipost picha yake ya wakati ni ujauzito huku akii-tag akaunti ya mtoto wake huyo na kuandika “Goodnight ? .Thank U for this outfit love @fifi_sugardesign . Love U baby dee @abdulnaseeb_tz,”
Wiki iliyopita kupitia kipindi cha Shalawadu cha Clouds TV, mama Diamond pamoja na dada yake Diamond, Esma walionekana katika nyakati tofauti wakiwa katika hospitali moja ambayo alijifungilia mrembo huyo.
Diamond ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul, hajatoa kauli yoyote juu ya mtoto huyo licha tetesi hizo kuonyesha zinaukweli ndani yake.
Kwa sasa muimbaji huyo ambaye ni rais wa WCB, ni baba wa watoto wawili aliozaa na Zari The Bosslady.