-->

Janjaro Aanika Maisha Yake, Kuonja Penzi la Uwoya!

MOJA kati ya headline zilizosumbua kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni ni uhusiano wa kimapenzi kati ya chalii wa Ngarenaro-Arusha, Abdulaziz Chende ‘Dongo Janja’ na staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya.

Umri wa Dogo Janja ambaye pia utakuwa hujakosea kama utamuita Janjaro umeshapita miaka 18. Ana uhuru wa kuingia kwenye masuala ya uhusiano, lakini suala la msingi ni kumpata mtu sahihi. Je, anatembea na mtu sahihi? Anaweza kusubiri umri usogee zaidi ndipo aingie kwenye masuala ya uhusiano? Jibu analo mwenyewe bwa’mdogo huyu aliyejizoelea umaarufu kwa ngoma kali kama Ukivaaje Unapendeza, My Life, Kidebe na nyingine kibao.

Dogo Janja au Janjaro ni miongoni mwa wasanii wenye umri mdogo ambao wameutendea haki muziki wa Hip Hop na amefanikiwa kuwa kwenye headline karibu kila siku. Janjaro, kwenye makala haya, amezungumzia ishu mbalimbali zinazohusu maisha yake ya kimuziki na uhusiano. Twende pamoja;
MCHANGO WA MADEE KATIKA MUZIKI WAKE

“Madee ana mchango wa asilimia 99 kwenye mabadiliko yangu ya kimuziki. Amekuwa siyo tu msimamizi wangu, amekuwa mtu mwenye uchungu na muziki wangu yaani mpaka ukiona wimbo unatoka, ujue tumebishana sana na yeye atakayoamua ndiyo inatoka na mimi huwa naamini sana sikio lake.

KUHUSU MAFANIKIO NA JINA LAKE

“Ukuaji wa jina na kipato Kibongobongo bado na sasa hivi siwezi kuzungumzia mafanikio kwa sababu bado nayatafuta kwa hiyo ninachoshukuru ni kwamba kidogo ninachokipata kinanitosha. Kinanifanyafanya nisichoreke na ninaishi maisha yangu kwa usawa wangu.

PLANI ZAKE KUHUSU FAMILIA

“Kwa ndoa bado ila nahisi nitapata mtoto kwanza before (kabla) ya ndoa. Ila nitazaa na mtu ambaye nimeona future (malengo ya muda mrefu) kwake.

WIMBO WA MY LIFE NA ASILIMIA ZAKE KATIKA MAISHA YAKE
“Nilichokiimba katika wimbo wangu wa My Life kina ukweli halisi katika maisha yangu kwa asilimia kama 75 hivi, hivyo ukiusikiliza wimbo huo utapata asilimia 75 ya maisha yangu halisi.

KWA NINI AMEBADILIKA KUTOKA HIPHIPO KWENDA REGAE?

“Muziki ni mabadiliko. Popote pale ulipo ukihitaji kufanikiwa lazima kuwe na juhudi za kujiongeza na mabadiliko vinginevyo utabaki kuwa nyuma kila siku.

MPANGO WA KUFANYA SINGELI…

“Sijafikiria bado kufanya singeli. Siwezi kupita mlango ambao umeshatumika. Mimi nakuja kuwasapraizi watu na kitu kngine kabisa. Mashabiki wangu nataka wasinizoee. Yaani nakuja na kitu tofauti. Siwezi kuja na singeli ambayo wameshafanya kaka zangu akina Prof Jay na wengineo.
IDEA YA UKIVAAJE UNAPENDEZA…

“Ile idea bwana ilikuja baada ya kugundua mimi ninapendeza kuliko wasanii wote wa kiume. Nilipoona hivyo nikaona kumbe ninaweza kuandikia mashairi. Nikafanya hivyo na ndiyo ngoma ikatoka na kama ulivyoona imependwa na wengi.

MIPANGO YA KUACHIA NGOMA HIVI KARIBUNI VIPI?

“Tuna utaratibu wa kuachia ngoma mimi na bro Madee. Hivyo mimi ni muda wa kumuachia Madee. Kwa sasa ni zamu ya Madee. Ameachia wimbo mmoja mkali sana Ijumaa hii (iliyopita) unaitwa Sikira ambao amefanya na Tekno kutoka Nigeria.

UKWELI KUHUSU KUTOKA NA UWOYA

“Hamna ukweli wowote pale kati yangu mimi na Uwoya. Uwoya yule ninaheshimiana naye sana, siwezi kufanya kitu kama hicho hata siku moja. Hayo mnayoyasikia yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii ni uzushi tu. Wanaendeleza tu maneno niliyowahi kusema kuwa ninamkubali kinoma…”

WANA PROJECT YOYOTE NA UWOYA?

“Yaani kama nilivyokwambia, Uwoya ni mwana tu ambaye ninaheshimiana naye, kamwe siwezi kufanya kitu cha ajabu na hata yeye mwenyewe anajua ni jinsi gani ninamheshimu.”

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364