Johari kutinga bungeni 2020
Blandina Chagula maarufu Johari mwanadada ambaye amewahi kutamba kwenye tasnia ya maigizo na filamu nchini ameweka wazi kuwa ana mpango wa kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Johari ambaye kwasasa ni mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya filamu ya RJ huku yeye akiwa hashiriki sana kwenye filamu kwasasa kama muigizaji amefunguka kuwa muda ukifika ataeleza nia yake.
”Nina mpango wa kugombe Ubunge, nia ninayo ila ni vitu ambavyo vipo kwenye mchakato na vikiwa tayari nitaviweka wazi”, amesema kwenye Kingaangoni ya EATV.
Kwa upande mwingine Johari amesema kushiriki kwake kwenye siasa ikiwemo kumsaidia msanii mwenzake Irine Uwoya ambaye alikuwa anagombea ubunge wa viti maalum Tabora haikuwa kwaajili ya maslahi bali alifanya kwa mapenzi.
Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoani Shinyanga, amekuwa mwanachama na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na amekuwa akishiriki katika mambo mbalimbali ikiwemo mikutano mikubwa na kampeni za uchaguzi.