-->

Johari: Ndiku Alitupa Raha

BLANDINA Chagula ‘Johari’ amemfungukia aliyekuwa mume wa muigizaji Irene Uwoya, marehemu Hamad Ndikumana kuwa enzi za uhai wake, aliwapa bata za kutosha.

 

Akizungumza na mwanahabari wetu hivi karibuni, mkongwe huyo wa sinema za Kibongo, alisema Ndiku alipokuwa anakuja nchini akitokea nchini Cyprus alikokuwa akiishi, alikuwa akiwaletea zawadi na kujirusha naye sana.

“Kama unavyojua mimi na Irene ni damudamu, alikuwa anatupa raha hatari. Kuna wakati tulienda naye hadi Cyprus tukala raha sana, kwa kweli Ndiku ana roho ya peke yake, Mungu amlaze mahali pema peponi, amina,” alisema Johari.

Ndikumana ambaye alibahatika kuzaa mtoto mmoja na Uwoya kabla hawajatengana, alipatwa na umauti wiki iliyopita nchini kwao Rwanda kwa maradhi ya moyo.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364