-->

Joketi Mwegelo Anavyotamani Watoto Mapacha

MWANAMITINDO na msanii maarufu nchini, Joketi Mwegelo, ameweka wazi kuwa anatamani kuwa na watoto mapacha katika maisha yake.

Joketi Mwegelo

Joketi aliweka wazi hayo alipotembelea Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, inayochapisha magazeti ya MTANZANIA, BINGWA, DIMBA na Rai, zilizopo Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam.

Joketi ameweka wazi kwamba mwanamume atakayekuwa mume wake atamuweka wazi hivi karibuni lakini anapenda wawe na watoto mapacha atakaowalelea kijijini.

Jokate ambaye pia ni maarufu kwa jina la Kidoti ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Kidoti, alisema: “Kuna umri ukifika unajikuta unatamani kupata mtoto, napenda nipate watoto mapacha na wote niwalee maisha ya kijijini na mjini ili wajue maisha ya pande zote.

“Napenda niwalee watoto hao maisha ya kijijini ili wajifunze kilimo, kula chakula vya asili na wajifunze tabia nzuri na za kupendeza jamii,” alieleza Kidoti.

Akizungumzia kuhusiana na muziki wake, Miss Tanzania huyo namba mbili mwaka 2006 na Kaimu Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, alisema hajasainiwa katika lebo ya muziki inayoitwa King Music inayomilikiwa na Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Salehe maarufu Ali Kiba.

Licha ya kutokutoa wimbo kwa muda mrefu, alisema hakuwahi kusainiwa kwenye lebo hiyo na taarifa hizo naye amekuwa akizisikia kupitia redioni.

“Alikuwa anafikiri hivyo lakini mpaka sasa hajanipa mkataba wowote nami nilisikia tu kwenye redio kwamba nipo kwenye lebo yake lakini hajanisainisha, labda bado anajipanga,” alisema Jokate huku akitabasamu.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364