Kalapina Akana Kutafuna Mamilioni ya Chid Benz
Msanii wa Hip Hop na mwanaharakati wa madawa ya kuleva Kalapina amekanusha tetesi za kutapeli milioni 50 zilizotolewa na wadhamini kwa ajili ya kumsaidia Chid Benz kuachana na madawa ya kulevya.
Akiongea kupitia eNewz Kalapina amesema hakuna mtu yeyote aliyejitokeza na kutaka kumsaidia Chid Benz bali alijitolea na kupoteza pesa nyingi alivyokuwa anakwenda kumsalimia Chid Benz alipokuwa Soba House.
Hata hivyo Kalapina amesema suala la madawa ya kulevya limekuwa kama ugonjwa wa Taifa kwani asilimia kubwa ya vijana wanajiingiza katika janga hilo hivyo ni vyema kwa viongozi wa serikali na jamii nzima kuwekeza na kuwezesha wanaharakati ili kuokoa jamii nzima.
eatv.tv