-->

Pichaz: Dua ya Sajuki Ilifanyika Songea

Siku ya tarehe 31/12/2016, muigizaji  Wastara Juma alimfanyia dua marehemu mumwe wake, Sajuki huko mkoani Songea.

Wastara alifunguka haya;

“Naanza kwa kumshukuru mungu wangu anaenipa pumzi ya bule mpaka mda huu
Sina budi kusema haya nitakayoyasema kwa ajili mwaka mpya unaonza kesho.
Ni miaka 5 na miezi 6 leo imetimia toka furaha yangu ilipoingia dosari, Mungu alinipa mtu wa kunipa furaha kwasababu kilakitu Alhamdulilah nilikuwanacho kulingana na nafasi yangu lakini sikuwa na furaha lakini furaha hiyo aikudumu nakumbuka ilikuwa mwezi 6/ 2011 marehemu sajuki alipoanza kuumwa ndipo furaha ilipoanza kupotea kwa sababu sikupata nafuu wala moyo wangu kupumzika mpaka leo tarehe 31/12/2016.

Nimejaribu kutafuta furaha kila sehemu kila njia ila imeshindikana, kuishi katika mazingira hayo kwa mtu mwengine angekuwa kama kizee hata kuchana nywele ingekuwa shida ila katika maisha ya maumivu na sajuki siku moja aliniambia mke wangu mi naumwa ila sipendi kukuona ukiwa mchafu na pia usinizuie kwenda kokote sababu nitakufa siku yoyote tutumie mda uliobakia kufanya kile kitu moyo unataka.

Nami kwasasa naishi hivyo nahisi mauti yapo karibu yangu sana hivyo kile moyo wangu unataka ndicho nakifanya hata moyo ukiniambia inuka na maumivu yako nipeleke baharin basi naupeleka uko ukisema nipeleke disco naupeleka uko ukisema nikakeshe msikitini naupeleka uko hivyo sitabariki na sipendi kuishi ili mtu anione nina maumivu nalazimisha furaha japo aipo hivyo mnisamehe wale wote msionielewa kokote mkinikuta mniche tu sifanyi kitu kumkera mtu i need peace of mind,moyo wangu maskin unanivuja damu kilasiku natamani nifanye lolote ili upumue hakuna kitu kibaya kama kupoteza furaha na tumain unaishi kama uko dunia ya peke yako nimeongea haya ili muelewe hisia zangu kuwa hata ukiongea kitu ambacho sijakifanya sihusiki au kunitafsiri vibaya naumia mara 2 nahisi kama na wew ni mmoja ya wale wasiopoenda kuona nikifurahia uwepo wangu duniani.
Viongozi wangu ndugu jamaa wasanii wenzengu na mshabiki wangu nawaomba kwa pamoja mpige goti kuniombea 2017 moyo wangu upate furaha ya kudumu upate dawa ya maumivu upate tabasamu la kweli na sio feki ninalotoa sasa aniondoshee maradhi yote.
Moyo wangu unahitaji furaha masikin mwaka 2017 uwe na neema kwetu sote ameen
kumpata kma wew aiwezekani basi hta mfano wako tu!!toka kuondoka kwako nimekuwa sikauki machozi na maumivu, Mungu akulaze mahali pema” –wastara

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364