-->

Kamanda Sirro Amtaja Vee Money Ishu ya Madawa, Atakiwa Kuripoti Kituoni Jumatatu

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amemtaja msanii wa Bongo Fleva, Vanesa Mdee ‘Vee Money‘ kuwa ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kuhusika na mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya baada ya jina lake kuongezwa kwenye orodha iliyotajwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kamanda Sirro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa kuhusu wasanii walioitikia wito wa RC Makonda aliyewataka wasanii 9 na askari polisi aliowataja kutuhumiwa kuhusika na biashara hiyo wafike katiika Kituo Kikuu cha Polisi Dar leo kwa ajili ya Mahojiano.

Aidha Sirro amemtaka Vee Money kuripoti katika Kituo hico siku ya Jumatatu ijayo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Sirro ameeleza kuwa ni watu watano tu ambao ni wasanii na raia wa kawaida ndiyo wameripoti leo kati ya wale waliotajwa jan.

Mbali hna hivyo, Sirro ametoa agizo kwa polisi kuwa, wale ambao hawajaripoti, watafutwe na wakamatwe hadi kufikia Jumatatu.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364