-->

Wema Sepetu: Situmii Madawa ya Kulevya

Wema Sepetu anataka kuweka jambo moja ‘very clear’ kuwa yeye si mtumiaji wa madawa ya kulevya.

Wema Sepetu

Staa huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwenye orodha ya mastaa wanaotuhumiwa kubwia unga na walioamriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujisalimisha kituo cha polisi central jijini Dar, Ijumaa hii kwa mahojiano zaidi.

“Mimi kama Wema nimekuwa nikisemwa sana kuhusu kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kujihusisha katika kuuza madawa ya kulevya,” amesema Wema kupitia app yake.

“Sometimes wanasema nimefungwa, sometimes nimenyongwa, sometimes nimekamatwa hususan pindi ninaposafiri kwenda nchi mbalimbali, na sasa hivi nimeambiwa kwamba natumia madawa ya kulevya. Well, ni habari ambazo mheshimiwa mkuu wa mkoa amesema hana uthibitisho nazo lakini amelazimu kutaja majina kadha wa kadha ambayo ndio hivyo ameyataja mengine kwenye vyombo vya habari, na ameamuru twende tukaripoti kesho (leo Feb 3), ifikapo saa tano asubuhi,” ameongeza.

“Mi nasema hivi, nitaenda, nitaripoti, kwasababu ni wito ambao ametaja mkuu wa mkoa wangu kuona amefanya, unaambiwa kubali wito, usikatae neno. Kwahiyo tutaenda kesho, na ntamsikiliza yale ambayo anataka kuniambia, iwapo tukishajua which is true, which is not, then tutajua from there what to do, sasa hivi sina cha kusema, sina cha kufanya, because bado sijaonana naye, kwa sasa niacheni tu nirelat but I want to assure you one thing, I am not a drug addict, and I am not a drug abuser, and if I was nadhani we all know how drug addicts act, we all know how drug abusers wanakuwaga. I want you guys to relax, do not worry, everything is going to be fine.”

Mastaa wengine waliotajwa ni TID, Mr Blue, Chidi Benz, Recho na wengine.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364