Kawele: Wanawake Kubweteka ni Kununua Umasikini
MKONGWE wa filamu Tanzania, Grace Mapunda ‘Mama Kawele’, amesema wanawake wanaobweteka ni sawa na kuununua umasikini.
Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema miaka kadhaa iliyopita na sasa hivi ni tofauti, mwanamke wa sasa anatakiwa asiangalie upande mmoja bali asimame kama nguzo katika familia na kuhakikisha anautokomeza umasikini wa kujitakia.
“Wanawake wanaobweteka bila kujishughulisha na kuukubali umasikini kiukweli wananiumiza sana kichwa na sipendezwi na tabia hiyo, maisha ya sasa yamebadilika hakuna mtu anayependa ategemewe kama zamani, wote inatupasa tuutokomeze umasikini kwa kuungana na kushirikiana hata kwa kuuza mboga,” alisema Kawele.
Msanii huyo aliongeza kwa kuwataka wanawake wabadili mtazamo wa maisha na wanatakiwa kujitambua zaidi.
Mtanzania