-->

Khadija Kopa Naye Sasa ‘Aisoma Namba’

Msanii wa taarab Bongo, Khadija Kopa ni kama naye sasa ‘anaisoma namba’ baada ya kutoa kilio chake juu ya kupungukiwa na mapato yatokanayo na muziki na kutaja sababu mojawapo kuwa ni uamuzi wa serikali kuzuia matamasha ya muziki baada ya saa 6 usiku.

Khadija Kopa

Amesema hivi sasa yeye na wenzake wapo katika mpango wa kuongea na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ili aangalie upya sheria iliyowekwa ya kufunga sehemu za starehe saa sita usiku kwa kuwa inawaumiza wasanii wa taarabu.

Amesisitiza kuwa kwa sasa biashara ya bendi za taarabu imekuwa ngumu na wanakosa mashabiki kwa kuwa muda wa kutumbuiza umekuwa mchache hivyo wanajipanga kuomba kwa mkuu wa mkoa ili siku za Ijumaa na Jumamosi ziongezewe  muda hadi saa tisa usiku.

Khadija Kopa aliyekuwa akizungumza kupitia eNewz ya EATV, amesema sababu nyingine ni utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia majina ya wasanii wakubwa wa taarab kufanya show na kujiingizia kipato kisicho halali.

Hii ni ishara kuwa Khadija Kopa ambaye pia ni muimbaji wa wimbo wa ‘Wataisoma namba’ kupitia bendi ya TOT, naye sasa ‘anaisoma namba’.

Mtazame hapa..

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364