-->

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania

Rais John Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini.

Jenerali Venance Mabeyo

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana jioni inasema Mabeyo amechukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Davis Mwamunyange ambaye amestaafu. Mbali na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi, Mabeyo amepandishwa cheo kuwa Jenerali.

Pia, Rais Magufuli amemteua Meja Generali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mabeyo.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364