-->

Kidoa Afungukia Bifu Lake na Masogange Juu ya Staa Huyu wa Bongo Muvi

Video Queen maarufu hapa Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ ambae kwa sasa amejikita kwenye uigizaji, amefungukia swala la bifu kati yake na Video Queen mwenzake, Agnes Gerald.

kidoa02

Iliwahi kuripotiwa kuwa, Kidoa alikuwa kwenye bifu zito na mrembo  mwenzake, Agnes Gerald maarufu Masogange, kisa kikielezwa ni kugombea penzi la staa wa filamu za Kibongo, Rammy Galis; Kidoa anasema juu ya hilo?

“Ni kweli tulikuwa na bifu tena kubwa sana lakini tulikuja kukaa tukaelewana. Unajua ilivyo ni kwamba, mimi huyo bwana wake sikumtaka na wala sijawahi kutoka naye na kama ningemtaka basi mimi ningeanza kuwa naye kabla yake.

“Ukweli ni kwamba nilikuwa karibu sana na Rammy Galis kwa sababu ya kazi na mpaka sasa tumefanya kazi nyingi ambazo zimetufanya tuwe  karibu.

“Wadau wajue kuwa, sasa mimi na Masogange ni mashosti wa kupika na kupakua. Hatuna bifu tena, mambo yanakwenda. Tena kwa taarifa tu ni kwamba, katika mamodo wanaonisapoti zaidi, Agnes ni zaidi ya wote,” anasema Kidoa.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364