-->

KR Muller:Sipo tayari kumzungumzia Juma Nature

Msanii maarufu wa Bongo Fleva nchini KR Muller amesema hawezi kumzungumzia msanii mwenzake Juma Nature kuhusu kauli zake kwamba ana wasiwasi KR anatumia madawa ya kulevya.

KR Mullah2

KR ameyasema hayo katika kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV alipotakiwa kutoa kauli yake kuhusu tuhuma ambazo Juma Nature amekuwa akizitoa mara kwa mara kwamba yeye anatumia ‘sembe’.

“Tuzungumzie mambo mengine lakini mimi sitaki kumzungumzia Juma Nature kwa kuwa hayupo hapa mimi napenda nikimzungumzia mtu kitu nay eye awepo” Amesema KR.

Aidha KR Muller amewatoa hofu mashabiki wake kwamba wasihofu kuhusu picha zilizotapakaa akionekana amelala kwenye maeneo yasiyofaa na kwamba alikuwa amechoka kutokana na kazi anazofanya.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364