Kidoa: Nampenda Diamond Kiukweli
MREMBO anayepamba video za wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva, Asha Salum (Kidoa), ameweka wazi kwamba anampenda msanii Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) ndiyo maana anataka kufanya naye kazi.
“Nampenda Diamond Platnumz kwa kuwa ana mvuto na anajitambua anachofanya huku akithamini kipaji chake kwa kufanya kazi kwa bidii pia kitu ambacho kinanivutia kwake zaidi ni kuweza kuipeperusha bendera ya Tanzania kila kona,’’ alisema Kidoa huku akidai kwamba anatamani siku moja afanye naye kazi kwenye moja ya nyimbo za msanii huyo.
Mtanzania