Nitaandamana Kwa Filamu Nzuri – Gabo Zigamba
Muigizaji wa filamu bongo anayesifiwa kwa kufanya vizuri, Gabo Zigamba amefunguka na yeye maandamano yake anayafanya kwa kutengeneza kazi bora kwa mashabiki zake waliompa nafasi ya kuonekana a siyo kuhofia soko kushuka.
Gabo amefunguka na kusema kuwa katika kuhakikisha soko linasimama na kuwa imara yeye ameamua kutengeneza kazi nzuri haswa katika kipindi hiki ambacho wasanii ewngi wamekata tamaa na kufanya maandamano na kuongeza kuwa kila mtu ana njia yake ya kufanya mapinduzi ya soko.
“Ukimjua adui yako hutakiwi kumjulisha mbinu unayotaka kutumia kushindana naye, ni kweli soko siyo zuri lakini mimi maandamano yangu ndiyo haya hapa. Nipo location natengeneza movie ambayo na uhakika ni nzuri na hii kwangu ndiyo mbinu niliyochagua kumshinda nayo adui yangu” -Gabo alifunguka
Pamoja na hayo Gabo amewataka mashabiki wa filamu waendelee kuwapatia changamoto za kejeli ikiwa ni pamoja na kusisistiza kazi nzuri ili wasanii wasibweteke isipokuwa kutoa lugha za matusi
Kwa upande mwingine Gabo amefunguka kuhusu picha zake na muigizaji Wema Sepetu zenye mahadhi ya mapenzi zinazosambaa katika mitandao ni kutokana na filamu wanayoiandaa ni ya mtindo wa ‘Romantic’.
“Movie tunayoifanya na Wema iko very tomantic ndio maana hata picha zenyewe lazima ziwe hivo sasa watanzania naona wao washarasimisha kwamba kuna kitu kinaendelea kumbe hakuna pale tupo kazini na niwaahidi mashabiki zangu naanda kitu kikali sana mara mbili za jinsi wanavyonifahamu”– Gabo alimaliza kufunguka.