-->

Kilichomfanya Nahreel Apagawe kwa Aika, Hiki Hapa

Msanii na producer Nahreel amefunguka sababu kubwa iliyomfanya kumpenda mpenzi wake Aika, ambaye wanaunda naye kundi la Navy Kenzo kuwa ni kutokana na uzuri wa mashavu yake na siyo hips wala kifua kizuri.

Nahreel aliyasema hayo alipokuwa akiongea na EATV na kusema watu wengi wanadhani huenda alimpenda Aika kutokana na uzuri wake wa sura, uzuri wa umbo au uzuri wa kifua chake

“Watu wengi wanadhani nimempenda Aika kutokana na umbo lake au kifua chake hapana, kikubwa kilichofanya nimepende Aika ni yale mashavu yake na nimekuwa namtania sana hata usiku napolala huwa nayapiga piga sana, hicho ndicho kilinifanya nimpende Aika” alisema Nahreel

Mbali na hilo Nahreel anasema katika miaka 9 ya mahusiano yao Aika amekuwa msaada mkubwa kwake kufikia lengo lake la kuwa producer mkubwa na kumiliki studio kubwa yenye viwango kwani alikuwa anampa moyo na kumsukuma kufika ndoto yake hiyo.

“Leo nasema huenda nisingekuwa na Aika labda nisingekuwa hapa leo, haya mafanikio niliyopata katika kila kitu katika miaka tisa toka nipo naye ni kutokana na msukumo wake hivyo naweza kusema haya mafanikio tumejenga kwa pamoja” alisisitiza Nahreel

Kwa upande wake Aika anasema katika mahusiano yao changamoto kubwa huwa wanaipata katika kufanya maamuzi hususani maamuzi ya mwisho katika kitu chochote.

“Siku zote katika mahusiano yetu tunapata changamoto kwenye final decision ya kitu chochote kile, hapo ndiyo huwa tunapishana au kunakuwa na ugumu zaidi kwetu, lakini katika miaka tisa toka nipo kwenye mahusiano na Nahreel sina cha kujutia kabisa kwani tuna mengi ya kujivunia katika maisha yetu na maisha ya mtu mmoja mmoja” alisema Aika 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364