-->

Siasa Imechangia Kutuua Bongo Movie-Steve Nyerere

Mchekeshaji maarufu nchini Steven Nyerere amekiri kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa waigizaji kujiingiza kwenye siasa pia ni chanzo cha tasnia ya filamu nchini kupoteza mvuto.

Steven Nyerere

Steve amefunguka hayo ikiwa ni siku chache tangu kufanyika maandamano ya baadhi ya wasanii wa filamu kuishinikiza serikali kuwaondolea kodi katika filamu zao au kuhakikisha inakusanya pia kodi za filamu za nje ambazo zinakuwa zinapakuliwa katika mitandao kitu kinachopelekea kuua soko la ndani la filamu za bongo.

Steve ameongeza kuwa wasanii wenzake kwenda kupambana na wauzaji wadogo wadogo ni dhambi kwani kiini cha matatizo kipo kwao wenyewe  na hiyo yote imechangiwa na wasanii kuacha kazi zao na kufanya siasa.

Mimi naomba niongee ukweli leo, kilichotuawa bongo movie ni siasa. Kipindi tupo kwenye uchaguzi mkuu kulikuwa na makundi mawili ya siasa ambayo yalikuwa yanawasapoti wagombea tofauti ndani ya tasnia ya filamu. Lakini cha kushangaza uchaguzi tumeumaliza vizuri ila badala ya kuendelea na kazi zetu za uzalishaji wa filamu bado tunaendeleza kazi za watu ambazo hatuna hata utaalamu nazo“- alisema Steve Nyerere.

Pamoja na hayo Steve Nyerere ameongeza wapo wasanii wa filamu ambao wameweza kutenganisha siasa na filamu na kwamba hao ni wale ambao wamebahatika kuvaa kofia hizo mbili ndio maana wametumia busara zao kutotumika kwenye maandano ya watu wachache.

Unajua pamoja na siasa kuna watu pale bongo movie wana kofia mbili mbili mfano mimi niliwahi kugombea Ubunge wa Kinondoni kwa hiyo lazima najua nini nafanya, Irene Uwoya ni Mbunge pale na anayo nafasi yake ndani ya chama  ikitokea bahati mbaya mbunge wa viti maalumu akaanguka yeye ndiye atakayeziba pengo au Wema Sepetu na harakati aliozonazo sasa hivi na ndio maana hata ukiangalia kwenye maandamano watu waliyoyafanya wao walikaa pembeni siyo kwamba siyo wasanii , hapana ni wasanii ambao wamejitambua na hawataki kutumika kwa maslahi ya watu wachache“- Steve alimaliza.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364