King Crazy GK Aukacha Rap, Akijita Kuimba
Rapa kutoka kundi la East Coast, King Crazy GK ameamua kuingia Studio kwa Alonem ambapo amebadili maudhui ya uimbaji wake kutoka kurap na kufanya muziki wa kuimba huku video akiifanya na muongozaji Donald kutoka Uganda.
Akipiga story ndani ya eNewz, GK amesema kuwa ushindani uliopo kwenye game la muziki tofauti na zamani ikiwa ushindani ulikuwa wa hapa tu nchini, Ila kwa sasa wameongezeka wasanii mbalimbali wanaotoka hata nje ya nchi ya Tanzania.
“Nimeamua kuimba lakini ni kutokana na game la Tanzania kubadilika, zamani tulikuwa tukishindana sisi wa Tanzania kama Juma Nature, AY na wengine lakini kwa sasa muziki wa Bongo ume’change’ na kuingia mpaka wakina Wizkind, so kubadilika muhimu” amesema GK.
Hata hivyo GK amebadilisha kabisa aina ya muziki wake na kutengeneza ngoma yenye mahadhi tofauti kabisa na muziki wake huku mwenyewe akisema anaandaa mashambulizi makali ili kupambana na game la sasa.