-->

Masanja:Nimeoa Kuhamasisha Vijana Wasiogope

Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ aliyefunga ndoa hivi karibuni na kuzua tafrani kwa wasanii wenzake kutiwa hatiani kwa kutumia sare za askari siku ya harusi yake na mkewe Monica Masatu amefunguka kwa kusema kuwa amefungua njia kwa vijana wengi wenye uwezo kimaisha lakini hawataki kuoa.

MASANJA345

Masanja na Mke Wake

“Unakuta kijana yupo safi kimaisha lakini hataki kuoa hela anayo kila kitu anacho na anakuwa na viburudisho lakini kuoa hawataki sasa mimi nimewaonyesha njia sasa ole wake kijana mwezangu asioe na kuwachezea mabinti nitatoa displine,”alisema Masanja.

“Nikiona kijana ana uwezo halafu hajaoa ni bakora tu hadi waache kuwachezea mabinti wa watu, nimeanza na kijana kutoka Dodoma nimemchapa viboko vya kutosha,”

Harusi ya msanii huyo ilijaa burudani kuanzia kutoka kanisani ilipofungika katika kanisa la Mito ya Baraka baada ya kufungwa ukumbini wasanii wenzake Joti, Wakuvanga na Mac Reagan walitoa show huku wakiwa wamevaa sare za Polisi ambazo zimelifanya jeshi hilo kutoa tamko na kuwahoji wasanii hao kwa tukio la kutumia kitendea kazi chao.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364