-->

Kisa Riyama, Mwanaheri Achaniwa Nguo!

Msanii wa filamu anayekuja kwa kasi Bongo, Mwanaheri Ahmed hivi karibuni alikumbwa na dhahama alipokatiza Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar baada ya kuchaniwa dera lake kisa kufananishwa na muigizaji mwenzake, Riyama Ally.

mwanaheri32

MwanaHeri

Akizungumza na Amani Mwanaheri alisema kuwa, amekuwa akikutana na sintofahamu kubwa njiani baada ya watu wengi kumfananisha na Riyama hata kabla ya yeye kuingia kwenye uigizaji wa filamu.

“Aisee hivi majuzi watu walichana mkono wangu wa dera wakiwa wananivuta na kuniita Riyama huko

Kariakoo na hata siyo hivyo tu hata kabla sijaingia kwenye tasnia ya filamu wengi wananifananisha naye,” alisema Mwanaheri anayebamba na filamu yake ya Mwanaheri.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364