-->

Kisa Wivu Snura Awatosa Mastaa

MWANADADA mwenye umbo matata anayesumbua kunako Tasnia ya Muziki Bongo na Filamu, Snura Mushi ‘Snura’ amesema kuwa yeye ni mwanamke mwenye wivu sana jambo ambalo limemsababisha mpaka kushindwa kut   oka kimapenzi na mastaa wanaomtaka.

Akipiga stori mbili tatu na Uwazi Showbiz, Snura aliongeza kuwa amekuwa akifuatilia uhusiano wa kimapenzi wa mastaa wengi na kugundua kuwa huwa haudumu kutokana na mastaa kutokuwa waaminifu au mazingira ya kazi zao ambayo kwa wasanii wa kiume yanawafanya kuwa karibu na wanawake jambo ambalo kwake hawezi kulivumilia maana atahisi tu anasalitiwa.

“Naomba niwe muwazi, kwa sasa sitamani kabisa kutoka kimapenzi na mtu maarufu au niseme tu staa kutokana na mimi kuwa mtu mwenye wivu sana, unajua mastaa wengi wa kiume huwa karibu sana na wanawake kwa mazingira ya kawaida ya kikazi, sasa mimi nikiona hivyo ninafahamu ninasalitiwa tu,”alimaliza Snura.

Chanzo;GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364