Koletha: Kulea ni Kazi Ngumu
SIKU chache baada ya kujifungua mtoto wa kike, msanii mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Koletha Raymond amefunguka kuwa tofauti na alivyowahi kufi kiri, kulea ni kazi ngumu, hivyo kila mtu anapaswa kumheshimu mama aliyemlea.
Akistorisha na Za Motomoto News, Koletha alisema kulea siyo rahisi kama watu wengi wanavyodhani au kama yeye alivyokuwa akifi kiri kabla hajapata mtoto, kwani ni kazi ngumu inayomtaka mlezi kumhudumia mtoto kila wakati tofauti na maisha kabla ya kuzaa.
“Ukweli kulea ni kazi ngumu sana, kwani kwa siku hizi chache tu nimeshaanza kuona ugumu wake, nawasihi wenzangu ambao hawajapata watoto wawaheshimu na kuwapenda sana mama zao, maana mpaka wamekuwa watu wazima, wamefanya kazi ngumu sana,” alisema Koletha.
Chanzo:GPL