-->

KR Muller Auzungumzia Tofauti Kati ya TMK Wanaume na Rada

Msanii wa muziki KR Muller amefunguka na kuuzungumzia utofauti uliopo kati ya label yake ya zamani TMK Wanaume Halisi ya Juma Nature na alipo sasa Rada Enterntainment ya TID.

Muimbaji wa Bongo Fleva TID akiwa na rapper KR Mullah

Muimbaji wa Bongo Fleva TID akiwa na rapper KR Mullah

Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni meneja wa label yake ya zamani TMK Wanaume Halisi, Juma Nature kudai msanii huyo ameharibikiwa baada ya kuhamia label ya TID, Rada Enterntainment.

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, KR amesema anafurahishwa na maisha mapya ndani ya Rada Enterntainment ya TID.
“Kusema kweli maisha ya Rada nimazuri sana,” alisema KR. “Mimi nashangaa hayo anayozungumza anayapata wapi. TMK haiwezi lingana na Rada, Rada inaongozwa kikampuni zaidi lakini TMK kushkaji zaidi. Pia TMK ipo mbali zaidi nawadau, kwa hiyo mimi naweza sema nipo salama Rada,”

Pia alidai alistop kuachia wimbo kutokana na haya mambo yanayoendelea lakini wiki mbili zijazo ataanza kuachia nyimbo.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364