Dude ni Meneja Wangu Tu – Ester Kiama
WASWAHILI usema kuwa raha jipe mwenyewe na aisifia Mvua imemnyea, haya yanajitokeza kwa mwigizaji wa filamu wa kike Bongo Ester Kiama pale anapojikuta akimsifia mwigizaji mwenzake Kulwa Kikumba ‘Dude’ kama ni meneja sahihi kwake kwani kuwepo naye katika kazi zake kumezaa matunda katika kazi hiyo.
Kama ningekuwa pekee yangu labda ingekuwa kazi ngumu sana hata kutengeneza filamu yangu ya Ngoma nzito sinema ambayo ni nzuri na bora kabisa, Dude ni meneja sahihi kwangu amenishauri vizuri kikazi na msaada mkubwa kwangu,”alisema Ester.
Siku za nyuma iliwahi kuripotiwa kuwa wasanii hawa wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini Ester anasema kuwa hizo ni hisia tu za watu lakini yeye na Dude ukaribu wao ni wa kikazi tu kwani wakati anaandaa filamu ya Ngoma nzito alitumia wasanii wengi ambao bila Dude wangemsumbua na asingefanikiwa.
Akiongea na FC amedai kuwa filamu yake ya Ngoma nzito inakaribia kutoka hivi karibuni akiigiza na kusimama kama mtayarishaji wa filamu ambayo imewashirikisha wasanii kama Kulwa Kikumba ‘Dude’ Ester Kiama, Irene Uwoya na wasanii wengine kibao wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu.
Filamu Central