-->

Kufeli kwa Baraka Mkono wa Mtu Wahusishwa

Msanii Baraka The Prince amemlaumu meneja wake wa zamani chini ya RockStar 4000 Seven Mosha pamoja na mpiga picha maarufu Mx Carter, kuwa ndio wanaohusika na kufelisha kazi yake mpya YouTube.

Baraka ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye eNewz ya East Africa Television, na kusema kwamba watu hao wawili ndio walikuwa na ‘access’ ya acount yake ya YouTube, hivyo wao ndio watakuwa wahusika.
Baraka ameendelea kwa kusema kwamba mara ya kwanza walimfanyia hivyo kwenye acount yake ya zamani ambayo ilikuwa inasimamiwa na RockStar 400, views zilikuwa zinapungua badala ya kuongezeka huku wengine waklimlalamikia kuwa hawaioni YouTube, hivyo aliamua kuifuta na kufungua mpya, na hata hivyo waliendelea kufanya hivyo kwa acount hiyo mpya.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364