Hussein Machozi Nusura Azikwe Hai
Msanii wa Bongo Fleva ambaye aliwahi kucheza soka kabla ya kuanza kung’ara kupitia nyimbo zake za Full Shangwe, Utaipenda, Kafia Gheto na nyingine, Hussein Machozi naye yaliwahi kumkuta makubwa.
Mbali na muziki, lakini ni mmoja kati ya wasanii ambao wana vipaji vya kucheza soka. Machozi anafunguka kuhusiana na tukio ambalo hatalisahau katika maisha yake:
“Kuna siku nikiwa mkoani Kagera katika uwanja wa mazoezi wa Kagera, wakati huo nilikuwa nikiichezea Kagera Sugar B, tulikuwa tunafanya mazoezi, kama kawaida, ikatokea kona, katika harakati za kuupiga mpira nikagongwa sehemu ya nyuma ya kichwa na mwenzangu, basi palepale nilipoteza fahamu na kuanza kutoka damu puani, masikioni na mdomoni.
“Kwa jinsi nilivyosimuliwa, ni kuwa baada ya tukio lile niliwahishwa Hospitali ya Kihaka muda huohuo huku wengi wakiamini kuwa labda nimefariki, nilipofikishwa hospitalini, daktari aliyenipokea naye aliamini nimeshapoteza maisha akalipitisha hilo kuwa nimeshafariki dunia.