-->

Kuishi na Majirani Vyema ni Funzo Kwangu – Duma

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Daudi Michael ‘Duma’, amefunguka na kusema kuwa kuishi na watu vizuri kumemfunza na kumfanya aone kuwa na umuhimu huo baada ya majirani na marafiki zake kumfanyia sherehe ya kuzaliwa mtaani kwake Mwananyamala, Dar es Salaam.

duma894

Daudi Michael ‘Duma

Akizungumza na eNewz mwishoni mwa juma lililopita, Duma, alisema amefurahishwa na kitendo cha marafiki na majirani zake kumfanyia sherehe hiyo ya kuzaliwa mtaani kwake na kujifunza kuwa yote hayo ni kutokana na kuishi nao vyema.

eNewz ilizungumza na Duma na alikuwa na haya ya kusema “Nimefurahi sana kwa party niliyofanyiwa nashukuru sana ila pia birthday yangu hii imekuwa fundisho kwangu kwa sababu kama ningekuwa sikai na watu vizuri sidhani kama wangeweza kunifanyia hivi, nashukuru sana kwa upendo waliouonesha kwangu siku hii ya leo”

Pia Duma alimalizia kwa kusema anatarajia kuachia filamu yake hivi karibuni kwa hiyo mashabiki wake tukae tayari

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364