-->

Kuolewa na Kuoa ni Ufungwa – Rayuu

MUIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Bongo movie Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amedai kuwa maisha ya ndoa yanahitaji umakini mkubwa sana na kabla ya mtu kuingia katika uhusiano hadi kufikia watu kuoana lazima kuwe na utulivu mkubwa sana kwani moja ya changamoto kubwa ni mama wakwe na mawifi.

“Kuolewa au kuoa ni ufungwa kuna wakati inabidi kila mtu amlinde mfungwa wake,ukichemka lolote linaweza kutokea na ndoa kuruka mbawa na kila mtu akibaki akijutia au kulia tu bila ufumbuzi wa tatizo,”alisema Rayuu.

Msanii huyu wa filamu na tamthilia wa kitambo anasema kuwa pale kila mtu anavyojua kuwa yupo katika kifungo ni wajibu wake kumlinda mfungwa wake ambaye anaweza kuwa mke au mume, kwa sababu changamoto kutoka kwa ndugu uchukua nafasi hata kama mnapendana kwa maneno ya wanandugu mnaweza kutengana.

FilamuCentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364