Kutoka na Mzee Siwezi-Shilole
Msanii wa muziki wa bongo fleva Shiloe alimaarufu kama Shishi Baby amefunguka na kuwataka wanaume ambao wanategemea wanawake kuvalishwa, kulishwa wabadilike na kuanza kufanya kazi ili wasitegemee tena wanawake kuendesha maisha yao.
Shilole anasema wanaume ambao wanapenda kutunzwa na wanawake ni wanaume sanamu, maana wanaume makini hawawezi kutegemea kulelewa na wanawake.
“Haya mambo hayatakiwi kuwepo, ndiyo maana unaona wanaume wengi saizi hawataki kufanya kazi yaani mimi nikulipie hotel, nikununulie nguo, sijui unataka nini mimi ninunue sasa wewe hapo utakuwa mwanaume au sanamu la mwanaume” alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole aligusia suala la wanaume ambao yeye hawezi kutoka nao na kusema wanaume wazee yeye hawezi kutoka nao kimapenzi
“Sema dah kutembea na mzee inahitaji moyo kweli kweli, mimi kiukweli siwezi hili jambo” alisema Shilole
eatv.tv