Kwa Mara ya Kwanza Bongo Movie Kuonyeshwa Kwenye Jumba la Sinema
Filamu ya Nimekosea wapi? Itakuwa ni filamu ya kwanza kufungua njia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Suncrest Cineplex Cinema lilopo Quality Centre jumatano hii.
Ni muendelezo wa Bongo Movie Premiere, ambapo mastaa na mashabiki wa filamu wanapata fursa ya kuitazma filamu kabla ya kuingia sokoni.
Akiongea na FC muandaaji wa filamu hiyo ya Nimekosea Wapi? , Man Fizo aliezeza;
“Namshukru sana Mwenyezimungu kwa kupata bahati hii nimetengeneza filamu kubwa na inaonyeshwa katika ukumbi wa filamu kwa hadhi kubwa, nipo na wasanii wakubwa Gabo zigamba na wengine,”anasema Man Fizo.
Ni kuanzia saa 1:00 ambapo wasanii watapita katika Red Carpet na kuingia ukumbi kwa ajili ya kuona sinema yenye ubora mkubwa.