-->

Kwaheri Mwaka 2017 Karibu 2018 Bongo Movie

MWAKA 2017 umekatika tukisubiria mwaka mpya 2018 zikiwa zimebaki siku kadhaa tasnia ya filamu kama ilivyo sekta nyingine ambazo zilikuwa na matukio ya kukumbukwa na kuagwa kwa kuukaribisha mwaka 2018 kwa matukio mapya katika ukuzaji wa tasnia ya filamu Swahilihood kwa waliojifunza wamejifunza na wale waliopoteza ni vema kujipanga kwa mwaka 2018.

Uwoya na Dogo Janja

Kulikuwa na mengi yaliyotokea si rahisi kuyaandika yote kwani muda hautatosha na kuyamaliza bali tutaweza kuandika baadhi yake tu ili kujikumbusha na kuwa nafasi ya kujikumbusha na kuanza mwaka 2018 kwa matumaini na nguvu mpya kama ilivyozoeleka kwa wengi.

SOKO
Soko la filamu limeshuka sana kama si kupotea huku lawama kubwa zikiwa ni kutokana na uzalishwaji na uingizwaji wa tamthilia kutoka nchi kama za Ufilipino, India, Korea na sehemu nyinginezo tena zikiwa zimetafsriwa kwa Lugha ya Kiswahili na kuziua sinema za ndani kilio ambacho kimekuwa kikubwa.

Kufuatia sakata hilo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) hivi karibuni iliendesha oparesheni wakishirikiana na Msama katika kuwakamata wale waliokuwa wakiuza sinema bila kuweka Stempu bila kujali zinatoka nje au ndani zoezi hilo limefanikiwa kwani nao sasa wanaweka stempu kazi za nje.

Kwa wauzaji wa filamu za nje kupata fursa ya kupata stempu na kuwa ni bidhaa halali hapo hali ya soko kwetu inakuwa ngumu zaidi kwani wasanii wenyewe wanakubali kuwa kazi za nje zina ubora kuliko za ndani kuanzi matayarisho na hata maudhui watengenezaji wamefanikiwa na kuwa na kaz bora zaidi.

Aidha msanii na mtayarishaji Madebe Lidai ndio anatamba sokoni kwa sasa baada ya kubadilisha mfumo wa utengenezaji wa Dvd na kuwa sawa na zile Dvd zinazouzwa kutoka Ulaya, lakini si hivyo tu pia anatoa katika mfumo wa series yaani kazi za muendelezo kama zifanyikazo katika Tamthilia hivyo kulishika soko na pengine kuinua soko japo safari bado ni ndefu.

WASANII NA SIASA
Ikiwa hali ya upepo wa kisiasa haujatulia wasanii nao wamejikuta wakiwa ni sehemu ya kuyumba katika uamuzi wao pale Wema Sepetu akitangaza kurudi CCM akitokea Chadema alikohamia akiwa na kesi yake ya matumizi ya madawa ya kulevya, kupitia mitandao ya kijamii na mmoja wa kiongozi wa chama hicho akipinga njia hiyo.

Wema Sepetu

Huku tasnia ya filamu ikihitaji njia zaidi ya kujinasua na kufikisha ndoto za wadau wake kupitia umoja wao naye Rais wa Shirikisho la filamu anajiingiza kwenye siasa na kuibuka mshindi nafasi ya Katibu mwenezi Mkoa wa Dar es Salaam, na haijajulina kama anaweza kuendelea na nafasi zote mbili kuzitumikia.

NDOA
Mwaka huu si haba kwa wasanii wa filamu walipata bahati ya kufunga ndoa zao aliyefungua dimba alikuwa ni Irene Uwoya akiolewa na kijana mdogo kabisa wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja japo hadi leo kuna sintofahamu kama wasanii hawa ndoa yao ni kweli au lah lakini bado wapo pamoja.

Mwanadada machachari katika sanaa Zuwena Mohamed ‘Shilole’ naye hakuwa nyuma pale alipofanikisha Ndoa yake na mpenzi wake Asharaf Uchebe, baada ya uhusiano wao kuvuma katika mitandao ya kijamii na kuwa tetesi kuwa Shilole atakuwepo naye na kuachana naye kama Nuh Mziwanda.

HARAKATI ZA SOKO LA FILAMU
Mwaka huu kuliibuka harakati mbalimbali wasanii na wadau wakijaribu kupigania hali ya soko la filamu za ndani, lakini hali ni tete kwani toka waziri Nape aondoke mwaka uliopita filamu za nje zimeendelea kushika soko na kuzifanya filamu za ndani kusuasua sokoni jambo ambalo limewafanya wasanii wengine kumzika.

Wasanii wakiwa katika maandamano kupigania kazi zao.

Hivi sasa soko limekwama kwani wasambazaji wa filamu za nje nao wameingia katika ulipaji wa kodi jambo linalowafanya wawe wauzaji rasmi kwani nao wanapatewa stempu za mamlaka ya mapato na kuwa ni kazi halali kuuzwa, kitu ambacho awali hakikuwepo.

Wasambazaji wa ndani wanajaribu kujipanga kwa mwaka 2018 kuja na njia mpya ambayo ni kutengeneza katika ubora wa juu na kuwafikia wanunuzi walipo pengine ndio itakuwa mbinu ya kuua soko la kazi za nje kutoka Korea na Ulaya.

Kuna wale wenye imani kuwa soko la filamu linarudi kwani wamegundua moja ya sababu kuwa makini katika utengenezaji wa filamu kwani matatizo yaliyokuwepo awali hayatakuwepo tena watatengeneza sinema nzuri zenye uhalisia na kushindana na kazi za nje.

MATATIZO KESI
matatizo yaliyoikumba tasnia ya filamu kwa mwaka huu wa 2017 ni mengi lakini ni pale muigizaji nyota Bongo Wema Sepetu akiwa msanii pekee kwa upande wa Bongo movie kuhusishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya na kufunguliwa kesi ambayo hadi leo hii haijaisha ikiendelea hadi hapo huku itakapotoka.

Kwa upande wa mwanadada Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu mambo hayakwenda sawa pale kesi yake ilipochukua sura mpya baada ya kusikilizwa kwa muda kidogo na kisha kutoka hukumu ya kesi ya kuua bila kukusudia iliyomtia hatiani na kufungwa kifungo cha miaka miwili Jela.

Lulu anaacha simazi kwa wapenzi wa kazi zake kwa kesi ya kuua bila kukusudia ya kifo cha muigizaji nguli katika tasnia ya filamu Bongo marehemu Steven Kanumba, hiyo ilikuwa ni tukio la kushtua kwa wadau wa filamu Bongo, pia mwaka huu muigizaji wa kimataifa Ramsey Noah alifika katika kaburi la msanii huyu na kuhani.

UZINDUZI
kwa mwaka huu uzinduzi wa filamu umechukua kasi kubwa pale ambapo hata majina yamekuwa yakibadilika kama tulivyozoea katika uzinduzi nyingi wasanii wakipita katika zuria Jekundu(Red Carpet) lakini wasanii wetu wamekuwa wakipita katika Zuria la Dhahabu na kuitwa (Golden Carpet).

Pamoja na ubunifu huo lakini hali imekuwa tofauti sana kwa mfumo huu ambao kwa wenzetu mara nyingi ufanya Premiere siku moja kabla ya sinema kuingia katika majumba ya sinema kama ni njia ya kufungua onyesho rasmi na kuendelea kuonyeshwa sinema katika majumba ya sinema.

Kuna jambo la kujifunza kwa mwaka ujao wa 2018 kwa kuhakikishia filamu zetu haziishii kuruka tu katika majumba ya sinema na kisha kurudi katika Dvd au kukaa nayo ndani tu bila kuisambaza kwa watazamaji, mwaka huu watayarishaji watajipanga.

Ni hayo kwa mwaka 2017 nikisema tumemaliza salama na tujipange kwa ajili ya mwaka mpya wa 2018 tukiwana afya furaha kwa ajili ya kufanya vizuri na kuikuza tasania yafilamu Swahilihood. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Filamucentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364