Labda Nina Mimba ya Wizkid – Gigy Money
Video vixen Bongo, Gigy Money amekanusha tetesi za kuwa na ujauzito.
Gigy Money ambaye ameamua kuingia kwenye muziki na sasa anatamba na ngoma ‘Papa’, ameiambia FNL ya EATV kuwa ndoto yake kubwa ni kutoka kimapenzi na msanii Wizkid kutoka Nigeria pengine hapo ndipo utapatikana ujauzito.
“Kipindi cha sasa hivi na Papa ndio nimetoa?, hapana, ujue mpaka yananishtua maneno haya, you know sina mimba lakini labda nina mimba ya Wizkid unajua mimi natamani ikaenda ikashuka tu,” amesema na kuongeza.
“Yeah namkubali, unajua dream sio wote wanatimiza ndoto zao, mimi nimetimiza ndoto yangu, nilisema Tekno moyoni siumeona huyu hapa akajaa,” amesema Gigy Money.
Bongo5