Sitegemei Kiki za Instagram-Shilole
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shilole amewatolea povu mashabiki zake kwa kuwataka kuacha kumkalili kuwa yeye bila ya kiki na kukaa mtupu hawezi kufanya vizuri katika kazi zake za kimuziki.
Shilole amebainisha hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live ‘FNL’ kutoka EATV baada ya baadhi ya mashabiki zake kumuona msanii huyo kutoa video ya wimbo wake mpya ya ‘kigori’ ikimuonesha akiwa na muonekano wa tofauti kabisa kuanzia mavazi yake mpaka uchezaji wake.
“Sikutaka skendo katika hii video, nilitaka kuwachukua wale ‘real’ mashabiki zangu, nimefanya video nzuri kama mtoto wa kitanzania yenye maadili mazuri kwa ajili ya kila mtu, sijakaa utupu kabisa kwenye ‘video’ hii kama watu walivyozoea. Kwa hiyo inabidi tuwabadilishe na ndugu zetu watanzania waweze kuelewa kuwa kuna ‘video’ hii inataka iwe hivi na nyimbo hii inataka hivi ‘so’ kuna nyimbo za matashititi. Tuanze kukubali muziki kwanza siyo lazima kila siku niwe Shilole wa fujo fujo tu“, alisema Shilole.
Pamoja na hayo, Shilole amedai video ya wimbo wake kutafanya vizuri katika mitandao ya kijamii ni kutokana na yeye kutokata viuno kama mashabiki zake walivyozea kumuona katika nyimbo zake za awali alizowahi kufanya.