-->

Lady Jay Dee Shabiki Namba Moja wa Asley

Dar es Salaam. Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee amekiri wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Aslay na huwa anamsikiliza mara kwa mara.

Komando Jide katika moja ya mahojiano na kituo cha habari anasema, Aslay ndio msanii anayemkosha kwa sasa sababu ana sauti nzuri ambayo huwezi kuisikia sehemu nyingine ila kwake.

“Naupenda wimbo wa Muhudumu na naweza nikakiri wazi kuwa Aslay ndio msanii ninaemkubali kwa sasa yupo vizuri,” alisema.
Aidha, Jide anayetamba na wimbo wa I Miss You, amesema ndani ya wiki hii watu wategemee video mpya ambayo amefanya na muongozaji Justin Campos.

“Nilisafiri kwenda South Africa kufanya hiyo video na muda wowote kuanzia sasa kitu kinaweza kuachiwa,”
“Katika wimbo hizo vesi za kuchana aliandika One The Incredible na katika korasi tulishirikiana na Domokaya na kitu kimewahi kutoka kama hivyo,” alisema.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364