-->

Linah Alala na Wizkid Hotelini

Imefichuka! Hatimaye ishu ya wanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, kudaiwa kulala kitanda kimoja na msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, imebumburuka.
Baada ya kuandamwa na skendo hiyo ya kutoka kimapenzi na Wizkid huku mashabiki wake waliyo wengi wakishindwa kuamini juu ya uhusiano huo, hatimaye sasa mambo yamevuja na kujidhihirisha kuwa kweli staa huyo alilala hotelini tena kitanda kimoja na Mnigeria huyo.

wiz45

Kikieleza kwa kujiamini, kiliweka wazi kuwa Linah alilala kitanda kimoja na staa huyo kwenye hoteli moja iliyopo Masaki, Dar, baada ya msanii huyo kutua Bongo kwa ajili ya kufanya makamuzi kwenye moja ya shoo zake alizokuwa ameletwa na promota King Solomon.

“Linah alilala na Wizkid, alikaa naye hadi siku anaondoka kulelekea Nigeria, na nikwambie ukweli uliyojificha ni kwamba, Linah kumbe ni siku kibao alikuwa akiwasilina na Wizkid kupitia mtandao wa Insta Direct, lakini hawakuwahi kuonana ila nafasi ya kuonana na kulala pamoja ilikamilika baada ya Wizkid kuja Bongo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kumwagiwa ishu hiyo, gazeti hili ‘lilicheki’ na Linah ambaye alikiri ‘kubanjuka’ na Wizkid huku akidai kwamba kuna mtu alifuta kila kitu kwenye simu yake hasa kilichohusiana na Wizkid wakati yeye alikuwa na mipango mingi naye.
Alisema kitendo alichofanyiwa na mtu huyo ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake kimemhuzunisha mno kwani ndoto zake za kufanya ngoma na staa huyo zimeyeyuka.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364