Lulu Atamani Kuzaa
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameweka wazi kuwa kwa umri alionao, imefika wakati na yeye anatamani sasa kuzaa.
Akizungumza na 4-Tamu hivi karibuni baada ya kubanywa maswali mawili matatu, Lulu hakusita kulizungumzia suala hilo la mtoto japo hakutaka kuweka wazi kuwa atazaa na nani.
“Natamani tu na mimi nipate mtoto sema ndiyo hivyo bado natengeneza mipango ya mimi kuwa mama tena mama bora,” alisema Lulu ambaye anatajwa kuwa na uhusiano na bosi wa redio.
Chanzo:GPL