-->

Lulu: Kama Ndoa Amepanga Mungu Ipo Tu!

STAA wa sinema za Kibongo ambaye pia alikuwa msanii wa kwanza kuigiza akiwa na umri mdogo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kwa mara ya kwanza amefunguka kila kitu chake hadharani ambacho wapenzi wake wengi wamekuwa wakijiuliza bila majibu.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Lulu amesema kuwa kujiamini ndiko kumemfikisha hapo alipo, ungana nami katika makala haya;

Over Ze Weekend: Watu wengi wamekuwa wakijiuliza unapata jeuri ya kujiremba na kuvaa nguo nzuri kila siku au ndiyo mambo ya mtarajiwa?

Lulu: Unajua siku hizi watu wame-kariri sana kuwa kila mtu akipendeza ni mwanaume, kwa hali ya sasa mwanaume gani anaweza kufanya hivyo kwa mwanamke bila kujishugulisha, kuna vitu ninafanya ambavyo wengi hawavioni ndiyo vinavyoniingizia pesa.

Over Ze Weekend: Kumekuwa na miluzi mingi kuhusiana na ndoa yako kila kukicha mara inafanyika mwezi ujao, mara vikao vimeanza unazungumziaje hilo?

Lulu: Nafurahi kweli kusikia hizo habari, hivi mtu anawezaje kila siku anakutabiria ndoa? Sasa nazungumza mwenyewe kama Lulu, hakuna kitu kama hicho, kama ndoa amepanga Mungu kwa mtu ipoipo tu.

Over Ze Weekend: Baadhi ya mastaa wenzako wanasema kichinichini kama unajitenga , huonekani viwanja kama zamani au pale Leaders mlipokuwa mkikutana na wasanii wenzako, liko vipi hili?

Lulu: Jamani kila kitu kina wakati wake kabisa hivi mimi ni sehemu gani sijakanyaga au kiwanja gani sijaenda mpaka wengine waliweka kabisa bango niisiingie kwenye kumbi za starehe, hivyo kuna wakati mwingine unahitaji kuyabadili maisha yako kabisa.

Over Ze Weekend: Mara ya mwisho kutembelea kaburi la Kanumba ni lini?

Lulu: Unajua Watanzania wanapenda kuona mtu akifanya kitu lazima aweke kama matangazo, huwa natembelea kaburi lake kama moja ya ibada kwa wafu na hata kumuombea kanisani lakini ni vitu vyangu binafsi sio lazima kila mtu ajue nafanya hivyo.

Over Ze Weekend: Zamani kulikuwa na tetesi kuwa Dk. Cheni alikuwa anataka kukuoa hilo nalo vipi?

Lulu: (Kicheko) Hicho kitu hakipo kabisa.

Over Ze Weekend: Mastaa wengi siku hizi wamefululiza kupata watoto vipi wewe una mzuka na hiyo hali?

Lulu: Sipendi kufanya kitu kwa sababu watu fulani wanafanya, hakuna mtu ambaye hapendi mtoto, lakini naona bado muda wangu haujafika tu.

Over Ze Weekend: Zamani nilisikia umeokoka mpaka ukawa unatembea na Biblia kwenye pochi, vipi mpaka sasa upo hivyo?

Lulu: Kuokoka ni kumuabudu Mungu kwa kila jambo na bado nafanya hivyo, lakini pia kuhusu kutembea na Biblia sasa hivi hayo mambo mbona hayapo, ukitaka mstari wa Biblia unaupata kwenye simu tu.

Over Ze Weekend: Mara nyingi picha zako ukipiga inaonekana kama umehamia kwa shemeji vipi kuhusu hilo?

Lulu: Hapana bado niko nyumbani kwetu, naona ni mtazamo tu wa watu.

Over Ze Weekend: Vipi kuhusu shule bado unaendelea?

Lulu: Nasubiria kidogo nataka niendelee tena hivi karibuni ambapo nitakuwa nachukua Shahada ya Rasilimali Watu.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364