-->

Madee Aumizwa na Picha za Chid Benz Mtandaoni

Madee ameonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya watu kumpiga picha Chid Benz na kuzisambaza mtandaoni.

Madee mwigizaji wa filamu ya Catherine

kupitia mtandao wa Twitter ametoa yake ya moyoni kwa kusema kuwa kitendo cha kumpiga picha rapper huyo na kumuanika mitandani ni kumdhalilisha.

“Hawa wanaompigapiga picha @ChidiBeenz na kupost kwenye mitandao yao lengo lao kubwa ni nini?mbona tunazid kumdhalilisha?au mnataka kiki?,” ameandika Madee.

Kuna uwezekanao mkubwa kauli hiyo ya Madee imekuja baada ya kuona kipandwe cha video alichopost Solo Thang kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na Chid Benz huku afya yake ikionekana kuzidi kuwa mbaya.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364