-->

Christian Bella Awachambua Diamond na Alikiba

Msanii wa Band maarufu kama mkali wa masauti Bongo Christian Bella amezungumzia timu ambazo ziko mitandaoni kati ya Alikba na Diamond kusema kuwa Alikiba ana uzuri wake na Diamond ana uzuri wake kwa kuwa kila mtu anafanya vizuri kwa upande wake.

“Diamond ana uzuri wake na Alikiba ana uzuri wake wote na mimi siko kwenye label ya Alikiba yeye ni mshikaji tu ila siwez sema Diamond ananizid eti tukikaa hapa kufanya voko hapana ila kwa upande wa Diamond hakuna aliyeamini kama angefanya hayo yote ni msanii ambaye anajituma sana ila kila mtu anafanya vizuri kwa upande wake” Amesema Bella

Bella amewafananisha wawili hao kama chumvi na sukari  “Ni kama sukari livyokuwa muhimu katika chai na chumvi ilivyokuwa na umuhimu katika mboga na hawa wasanii wawili wote wana fan base kubwa sana na mashabiki wa team Diamond na team Kiba wote wanaupenda muziki wangu”

Christian Bella kwa sasa amefanikiwa kufungua studio yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la KINGDOM na ni mmoja kati ya wasanii wenye mafanikio sana katika muziki wa band nchini.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364