Majambazi Wavamia Nyumba ya Q Chillah, Waiba Vitu vya Zaidi ya Milioni 2
Q Chila amethibitisha nyumba yake kuvamiwa na majambazi na wamefanikiwa kuiba baadhi ya vitu vilivyomo ndani ikiwemo laptop iliyokuwa na baadhi ya colabo zake.
Akiongea na Clouds FM, muimbaji huyo amedai kuwa thamani ya vitu vyake vilivyoibiwa ni kama milioni mbili au tatu.
“Watumishi wa shetani wameamua kufanya kitu cha kihistoria, siku zote wanarukaruka mmoja wawili tunapigiza nao kelele wanaondoka lakini this time wamekuja watu kama sita, saba au nane.
Wamekuja na mapanga, wamekuja na mafokolisti yale ya kufungua, wamekuja na gari moja nje sasa sijui walikuwa wanataka kubeba kila kitu?,” ameuliza Q Chila.
“Pale sebuleni mavitu mengine yote wamepita nayo na gym ya nondo ilikuwa tulichukua Mlimani kwa sababu ya exercise,” ameongeza.
“Wamepiga maplazma, wamepiga music system yangu nimetoka nayo South Africa, wamepiga laptop ambayo tayari mimi nilikuwa naangalia nafasi ya kujipanga na connection zangu.
Wamepiga piga hivi kama tatu point something au mbili point something wamepiga,” aliongeza.
JF