-->

Mama yake Irene Uwoya amlilia Ndikumana

Mama mzazi wa msanii Irene Uwoya ambaye ni mkwe wa marehemu Hamad Ndikumana aliyefariki usiku wa jana kuamkia leo, ameshikwa na uchungu kwa kumwaga machozi mengi na kusema kabla marehemu hajafariki alikuwa anawasiliana naye na alimtaka kuwa na subira.

Akiongea huku akilia kwa kwikwi na machozi yakimtoka, mama Uwoya amesema Ndikumana alikuwa ni zaidi ya mkwe kwake, na waliishi vizuri siku zote, na kumtia moyo kuwa atayavumilia yote ambayo alikuwa akiyapitia.

Ndikumana mimi sijui nianzie wapi, alikuwa mkwe wangu kipenzi alikuwa kama rafiki, alivuka hata ukwe, Ndikumana wangu mkwe wangu siku zote tumeishi nae vizuri, siku zote tumekuwa tukiwasiliana mpaka mwishoni hapa nilikuwa natoka safari, ananiambia mama naomba tuwe na moyo wa subira, mimi nitavumilia yote ya dunia lakini mimi ni mwanao mpaka naingia kaburini, na kweli mpaka anaingia kaburini, mwanangu mimi nilikuwa nampenda”, alisikika mama yake Irene Uwoya ambaye alikuwa akilia kwa uchungu.

Ndikumana alikuwa mume wa ndoa wa msanii Irene Uwoya na baadaye walitengana, na kisha Irene Uwoya kuolewa na msanii wa bongo Fleva Dogo Janja.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364