-->

Niliachana na Uwoya kwa ajili ya Ndikumana-Msami

Mwanamuziki wa bongo fleva nchini Msami Baby amefunguka na kusema wazi kwamba aliwahi kujuta kuwa na mahusiano na Irene Uwoya baada ya kujua kwamba anamuumiza aliyekuwa Mume wa muigizaji huyo, Marehemu Hamadi Ndikumana aliyefariki usiku wa kuaMkia jana huko Rwanda.

Msami amefunguka na kusema kwamba hakuwahi kumchukia Mwanaume huyo (Ndikumana)  na kwamba kutokana na heshima aliyokuwa anampatia ndikumana ilimfanya aamua kuvunja mahusiano  hayo.

Msami amesema kwamba baada ya kugundua kwamba Ndikumana anapambania Ndoa yake na Irene Uwoya alijihisi mkosaji kitendo kilichomfanya ajisikie vibaya na hata lugundua kwamba nikitendo kisichopendeza mbele za Mungu.

“Kuna kitu kiliniambia nachokifanya siyo sahihi, nilimwambia Irene wewe umefunga ndoa ya kikristo na mimi nimetumikia kanisani kwa muda wa miaka saba hivyo naijua vizuri dini,  kuendelea kumuumiza mwanaume mwenzangu sikuona kama kuna maana ndiyo maana nilirudi kwa Mungu wangu na kujutia makosa niliyoyafanya” Msami.

Ameongeza “Sikuwahi kumfuata Ndikumana kumuomba msamaha kwa sababu nilikuwa na mahusiano na mwanamke wake, lakini nilienda luongea na Mungu wangu kisha nikaungama dhambi zangu ndiyo maana mimi na Irene tukaendelea kuwa Marafiki lakini kusikia tena jamaa amefariki imeniumiza sana.

Msami ni mwanaume ambaye alitajwa kuwa na mahusiano na Irene Uwoya kwa muda mrefu ingawa wao walikuwa wakikanusha na baada ya kuachana Msami alikiri kwenye FNL ya EATV kwamba aliwahi kuwa kwenye  mahusiano na muigizaji huyo

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364