-->

Man Fongo: Bila Mimi Hakuna Kisingeli

Msanii wa Singeli Man Fongo ambaye aliibuka mshindi katika tuzo za EATV Awards kama msanii bora anayechipukia amefunguka na kusema kuwa hakuna muziki wa kisingeli bila yeye.

Man Fongo alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ na kusema kutokana na mapenzi aliyopata kutoka kwa mashabiki na kumuwezesha kupata tuzo ya #EATVAwards ameamua kuwashukuru mashabiki kwa kufanya show ya bure leo ambayo itafanyika kwa Ali Maua.

“Mungu mkubwa nashukuru kupata hii tuzo kwani sikuwepo nilikuwa India lakini kwa kuwashukuru mashabiki wangu nimeamua leo tarehe 30 kufanya show ya bure ili nijichanganye na watu wangu wa uswahilini na kufurahia ushindi huu. Bila ya mimi hakuna kisingeli ila kwenye show yangu leo utaweza kuona wasanii wengine wengi wa Singeli ambao pia wanafanya vizuri hivyo watu waje kwa wingi washuhudie vipaji vingine”. Alisema Man Fongo

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364