-->

Kadinda Akanusha Kugombana na Wema

MBUNIFU wa mavazi nchini, Martin Kadinda, amesema hana ugomvi wowote na nyota wa filamu, Wema Sepetu, kama watu wanavyodai.

Wema Sepetu na Martin Kadinda

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kadinda alisema watu wamezoea kukaa na kutengeneza mambo ambayo hayapo, yeye ni meneja wa Wema na ataendelea kufanya naye kazi kama kawaida.

“Watu wamezoea kuzusha kila kukicha, kwa upande wangu sijawahi kugombana na Wema, ila kuna watu wana uwezo mkubwa wa kutengeneza habari ambazo hazina ukweli wowote hasa katika mitandao ya kijamii,” alisema Kadinda.

Mbunifu huyo aliongeza kuwa kwa sasa yuko bize na kazi zake za kubuni mavazi kama vile ya harusi ambayo yanamfanya azidi kuwa maarufu.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364