-->

Maneno ya Mike Sangu kwa Mama Kanumba Baada ya Kumtambulisha Mrithi wa Mwanaye

Fredy Swai na Mama Kanumba

KUTOKANA na hivi karibuni mama wa aliyekuwa staa mkubwa wa filamu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kumwanika kijana Fredy Swai kuwa ndiye mrithi wa mwanaye, msanii wa filamu nchini, Michael Sangu ‘Mike’ (pichani juu) ameibuka na kusema mama huyo na watu wengi waache kumfananisha staa huyo na watu wa ajabu ajabu.

Mike Sangu

 

Akizungumza na Gazeti la Risasi Jumamosi, Mike alisema mama Kanumba amekosea kusema kijana huyo ni mrithi wa mwanaye kwani hajamzaa pia Kanumba anatakiwa kuenziwa kwa kazi nzuri alizokuwa akizifanya kwani aliweza kuitangaza sanaa ya filamu ndani na nje ya nchi na siyo watu wanavyojifananisha naye kwa kuvaa, kuwa na muonekano kama wake.

“Tunataka mrithi wa Kanumba kupitia kazi siyo sura wala muonekano maana tangu afariki tasnia ya filamu ndiyo ina hali mbaya sana hivyo tunataka mtu ambaye ataendeleza mema yake pale alipoishia, mama yake angekuwa anataka mrithi wa mwanaye basi angeendeleza ile kampuni yake halafu vijana wakafanya kazi hapo angepata mrithi lakini ndiyo hivyo imekufa,” alisema Mike Sangu.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364